Jumatano, 22 Februari 2017

NGONO KATIKA NDOA

Ngono katika ndoa 
Mungu aliumba ngono 
Mungu alipo umba mwanadamu (mwanaume na mwanamke) ali waumba kuwa na uwezo wa kufurahia ngono kama kielelezo cha upendo wa kibinadamu kati ya mume na mke. kinyume namawazo kuwa ngono ni chafu,au hata kwamba ilikuwa nidhambi ya asili ilivyo tendwa na adamu na hawa ,ngono ili umbwa na mungu ili ifulahiwe na mume na mke. Mungu ali agiza kwamba zaeni mkaongezeke mkaijaze nchi na kuitiisha,njia pekee kwao ambayo wange weza kuzaliana,ilikuwa muungano kingono.Iweje basi mungu aweze kuwalaumu kwa kufanya lile ambacho kwa asili amesha waagiza kufanya?
Dhambi ambayo adamu na hawa alitenda haikuwa ngono Bali kumkaidi mungu kwakula tunda lililo katazwa (tundaharisi la mti) katika biblia imesema wazi kwamba "mwanaume ata mwacha baba na mama yake naye ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja " Maneno hayo "mwili mmoja" nidhairi kuzungumzia muungano wa kingono.hivyo ngono ni eneo muhimu sana katika ndoa. Ila "kuwa mwilimmoja" ni zaidi sana ya kuwa tendo la kimwili au mchakato muhimu wa kupata watoto.huhu sisha mbadilishano wa mawazo na hisia kiasi kwamba roho inahusishwa vilevile na mwili
  
               Mpango wa mungu kwa muungano wa kingono
Kama ilivyo kwa shughuli au uzoefu mwingine wowote wa kibinadamu ngono ni lazima itendwe katika mipaka ya kimungu iliyowekwa na muumba mwenyewe.biblia husema katika waebrania13:4 hutupa kanuni muhimu sana kuhusu usafi wa ngono. Mstari huu husema "Ndoa na iheshimiwe na watu wote,na na malazi yawe safi; kwa mana waasherati na wazinzi mungu atawahukumia adhabu" Ngono ni yenye kufaa na njema lakini katika ndoa peke yake -mahali sahihi kwa ajili yake.halo.ngono imeelezwa kuwa ni yenye heshima na safna Mungu ahukumu wafanyao ngono Nije ya ndoa. Wale ambao wako katika ndoa na wanajihusisha na shughuli za kingono na yeyote mbali na wenzi wao wandoa,wanafanya uzinzi. Mungu ahukumu pia shughuli za kingono kwa wale ambao hawapo katika ndoa lakini wanafanya ngono, iwe na mtu ambaye yuko katika ndoa na mtu mwingine au ambaye haja olewa au kuolewa. Huu ni uasherati au ufisadi wa kingono. Mungu hutusihi kwakusema "Ikimbieni zinaa.kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyae zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili kwenu ni hekaru la roho mtakatifu aliye ndani yenu,mliyepewa na mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe ;maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni mungu katika mili yenu."
Watu walio katika ndoa wanapaswa kutafuta utoshelevu wa kingono kutoka kwa wenzi wao wa ndoa peke yake, kama kama ilivyo fundishwa katika mithali 5:15-20. Kufanya ngono nje ya ndoa ni uovu na dhambi hukalibisha tu hukumu na laana ya mungu. Ufisadi wa kingono una matokeo mabaya,na wengi wamekuta uliwapatisha hasara. Madhara ya kimwili ni magonjwa mbali mbali ya ambukizwayo kwanjia ya ngono, ukiwemo UKIMWI. Madhara ya kihisia huhusisha hisia za hata, aibu, kujilaumu na ugumu katika kuunda uhusiano wa ndani na mpenzi wa ndoa. Wale ambao hawajaoa au kuolewa wajiepushe na ngono mpaka watakapo la au kuolewa.

Ita endelea tukutane katika sehemu yapili katika somo letu nikusihi tu usikose kutembelea blog yetu kila siku uweze kujifunza mungu juu ya maisha yetu yakila  siku katika jamii yetu inayo kuzunguka kama una itaji ushari tupigie katika na mbali ya simu mudawote 0764939292 asante kwakuichagua jamiiyetuleo



 Please weit.......................